KUNDI la Tembo zaidi ya mia mbili wamevamia makazi ya wananchi wa kijiji cha Nyamatoke kata ya Mosongo wilayani Serengeti mkoani Mara na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazao mashambani.
Diwani wa kata ya Mosongo Bw Kefa Mgaya, amesema kuwa kundi hilo la tembo limesababisha hofu kubwa kwa wananchi wa kata hiyo.
Amesema tayari ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti imeharifiwa kuhusu wanyama hao kuvamia makazi ya wananchi na kwamba hadi jana jioni hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa kwa ajili ya kuwandoa tembo hao na kufanya tathimini kuhusu uharibifu ambao umesababishwa na wanyama hao.
Hata hivyo diwani huyo amesema kutokana na Temba hao kukatalia katika vijiji vya kata hiyo kwa siku nne sasa bila kuondolewa kuna hatari kubwa ya wananchi hao kuchukua hatua ya kuwashambulia wanyama hao kutoka hifadhi ya taifa ya Serengeti.