mradi wa five by twenty unaomilikiwa na kampuni ya coca cola.
Mratibu wa mradi wa 5 by twenty Braytoni Mkocha amesema kuwa mradi huo umelenga kuwasaidia na kuwafikia wanawake wajasirimiamali milioni tano dunia nzima ifikapo mwaka 2020.
Amesema kuwa mradi huo kabla ya kuwapa wajasiriamali mali vifaa vya kutendea kazi wanawapa kwanza elimu ya biashara na tayari mikoa zaidi ya saba wameshawapatia elimu pamoja na kuwapa vitendea kazi na mradi umelenga hasa kuwasaidia wa kina mama kutokana na kuwa wao ndio wenye changamoto nyingi katika familia.
Kwa upande wake mratibu wa vikoba katika mradi wa five by twent Sophia Mpunga amesema kuwa mradi huo umelenga kuwafikia wanawake elfu 33 na mia tano kwa Tanzania na walifikiwa mpaka sasa ni elfu moja mia tisa sitini na nane na kwa mkoa wa Iringa wamefikiwa wanawake 21.
Hata hivyo amesema kuwa kutokana na kuwa mtaji mkubwa kwa wanawake hao ni chupa za soda amewataka kujitaidi kuzitunza chupa hizo ili kuongeza uaminifu na kuweza kukuziwa mtaji zaidi.