Saturday , 3rd Dec , 2016

Wasanii wanaowania Tuzo za EATV leo wamefichua siri ya mafanikio yao mbele ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Kampasi ya Mlimani), huku wakiwataka wanafunzi hao kujiamini na kutumia vizuri kile walichonacho ikiwa ni pamoja na elimu yao

Wasanii wanaowania tuzo za EATV wakizungumza na wanafunzi wa UDSM katika ukumbi wa Nyerere Theatre 1, Mlimani

 

Wasanii hao wamekutanishwa na wanafunzi kupitia kampeni ya 'Ready To Work' ambayo inaendeshwa na Benki ya Barclays Tanzania ikiwa na lengo la kuwawezesha vijana hususani wanafunzi ambao wana matarajio ya ajira, kujiandaa vizuri kuingia kwenye soko la ajira.

Katika tukio hilo ambalo lilikuwa likirushwa LIVE kupitia EATV na EA Radio, wanafunzi hao wamepata fursa ya kuwauliza wasanii hao maswali, na wao kuwajibu huku wakieleza safari ya mafanikio katika sanaa.

Baadhi ya wasanii waliofika ni pamoja na Kajala Msanja, Daudi Michael, Lady Jay Dee, Feza Kessy, Shetta, Meya Shabani, Khadija Ally, Man Fizo, Racheal, Ruky Beiby. n.k

Zifuatazo ni picha za baadhi ya wasanii hao na ujumbe walioutoa

Shetta: Mungu ni wetu sote, ukifanya kazi kwa bidii utafika unakotaka

 

Feza Kessy: Wasichana, wasidhani uzuri unaweza kufanya mambo yawe rahisi, ingekuwa hivyo leo mimi ningekuwa na Beyoce. 

 

Joe Bendera (Barclays TZ): Tunawakaribisha wote mjiunge na mfumo wa ReadyToWork na ndiyo utakuwa mlango wa kupata ajira Barclays

Khadija Ally: Niliamua kucheza 'movie za action' kutokana umbo langu kuwa hivi, naonekana sina nyama, kwahiyo kwenye movie za 'masofa' ningeonekana siwezi. Kwenye Bongo Movie watu wanaothaminiwa zaidi ni wale wenye muonekano mzuri.

 

Bright: Suala la wasanii kuwa na 'Team' katika muziki naliunga mkono endapo mashabiki wana nia njema

Jay Dee: Kama una kipaji lazima uji'push' kwanza watu wakuone, kabla hujaomba msaada, mimi nilikuwa napiga simu redioni naimba.......Kuhusu mavazi ya wasanii, imani yangu kwenye madera haipo kwahiyo siwezi kuvaa madera kwenye nyimbo zangu... Kupitia muziki wangu nimeshafanya mengi na bado ninafanya mengi kwa jamii.... Hapa nilipo tayari najulikana kidunia "worldwide"

 

Gabo: Ukiwa unasoma kwa matarajio ya kwenda kuajiriwa, utaajiriwa kwenye kazi ambayo hujasomea....., Nisiwe muongo wala mnafiki, matumizi yangu ya akili ndiyo yamenifanya nifike hapa mnaponiona.........Tasnia ya filamu inasuasua kwa kuwa wasanii tuna umoja wa nyumbu, tuko 20 lakini simba mmoja anatutoa jasho 

 

Meya Shabani: Niliwahi kumuibia mama yangu pesa ili nirekodi movie ya vichekesho ambayo ndiyo iliyonitoa kupitia kwa Pastor Miyamba, ambaye alipoipata kazi yangu alinipigia simu nikiwa Kigoma, akaniambia "Wewe ni biashara" nikasafiri hadi Dar na mpaka leo niko kwenye EATV Awards

Daudi Michael akisimulia safari yake katika sanaa, asema alianza kuigiza baada ya kukasirishwa na movie moja ya kibongo, wakati huo akiwa dereva wa tax, alipoingia kwenye uigizaji alikatishwa sana tamaa ingawa kuna watu walikuwa wakimshauri afanye kazi hiyo kutokana na muonekano wake. "Nilikuwa najiangalia kwenye kioo naona naweza, kwahiyo nikajiamini kuwa naweza"

 

Kajala: Namshukuru sana JB kwa kuwa ndiye aliyenipa fursa nikaonekana

 

Ruky Beiby

Racheal Bithulo: Nilianza zamani sana uigizaji tangu 2007 lakini sasa hivi ndo nimeonekana, safari ni ndefu na ina changamoto nyingi, mafanikio yanahitaji uvumilivu

 

Feza Kessy (kushoto) na Lady Jay Dee

 

 

Wanafunzi wakiuliza maswali

David Rwenyagira mtangazaji wa EA Drive ya EA Radio ambaye ndiye aliyekuwa HOST wa shughuli ya leo akiwa na washiriki wa EATV Awards

 

 

 

Tags: