Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itajenga chuo mahiri cha kidijitali pamoja na kutenga fedha maalumu zitakazowezesha Wizara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kuzipatia mitaji kampuni changa zinazomilikiwa na vijana (startups) ili ziweze kukua na kushindana katika soko la kidigitali.
Rais Samia mesema hayo leo Ijumaa, Aprili 10, 2026 wakati wa uzinduzi ya minara 758 na maunganisho ya mkongo wa mawasiliano katika wilaya 85 pamoja na kukabidhi mkongo wa mawasiliano serikalini katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma.




