Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na Gavana wa Lagos State, pamoja na watu mashuhuri na wadau wa tasnia ya burudani nchini Nigeria.
Kupitia lebo hiyo mpya, Tiwa Savage amesema lengo lake ni kuwatafuta, kuwasaini na kuwasaidia wasanii vijana wenye vipaji ambao wana uelewa wa muziki na shauku ya dhati ya kuendeleza sanaa hiyo.
Hatua hiyo inatajwa kuwa sehemu ya juhudi za msanii huyo kuendelea kukuza vipaji vipya na kuchangia maendeleo ya tasnia ya muziki barani Afrika.

