Rais wa Marekani, Donald Trump, ametoa kauli ya kejeli na onyo kwa mshirika wake wa muda mrefu, Uingereza, kufuatia taarifa kuwa nchi hiyo inafikiria kutuma meli zake mbili kubwa za kubeba ndege za kivita (Aircraft Carriers) kuelekea Mashariki ya Kati.
Trump amemtaja Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, akimwambia kuwa msaada huo "hauhitajiki tena" kwani Marekani imekwishapata ushindi wa kijeshi.
Katika ujumbe wake, Trump ameiondoa Uingereza kwenye hadhi ya "Mshirika Mkuu" (Greatest Ally), akitumia neno "Once Great Ally" (Aliyewahi kuwa Mshirika mkuu), akidokeza kuwa uhusiano huo wa kimkakati umeanza kufifia.
Trump ameshutumu utaratibu wa washirika kujiunga na vita baada ya ushindi kupatikana, akidai kuwa Marekani imeshafanya kazi ngumu peke yake.
Trump amemwambia Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer kuwa Marekani haina shida na meli hizo mbili, lakini amesisitiza kuwa Washington itakumbuka kitendo hicho cha kuchelewa kutoa msaada.






