Tuesday , 10th Feb , 2026

Mwekezaji wa Simba SC, Mohammed “Mo” Dewji, ameibua mjadala miongoni mwa mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuhoji maendeleo ya mchakato wa mabadiliko ndani ya Simba SC ni wapi ulipo fikia.

Mohamed Dewji

Mo Dewji ametoa hoja hiyo kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Simba SC, mara baada ya viongozi wa klabu hiyo kumaliza mkutano wao, akiuliza kwa uwazi kufahamu mchakato wa mabadiliko umefikia hatua gani.

Hatua hiyo ya Mo Dewji imekuja siku ambayo viongozi wa Simba SC wamekutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katika mkutano maalum uliolenga kutangaza kampuni zitakazoshika zabuni ya kutengeneza kadi za kisasa za mashabiki wa klabu hiyo