Wednesday , 4th Feb , 2026

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Danny Murphy, amemkosoa Cristiano Ronaldo kwa kugomea mechi ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia kati ya Al-Nassr dhidi ya Al Riyadh kwenye.

Cristiano Ronaldo na Danny Murphy

Taarifa zinaeleza kuwa Ronaldo alikuwa hakuridhishwa na mtazamo wa PIF na utaratibu wa kugawanya fedha, hasa kwa Al Hilal kupewa kiasi kikubwa kabla ya Kombe la Dunia la Klabu, huku Al-Nassr ikipata kidogo.

Pia, Ronaldo alijaribu kuzuia kujiunga kwa Karim Benzema na Al Hilal, lakini mpango huo haukufaulu. Murphy amesema Ronaldo anazingatia maslahi yake binafsi badala ya klabu.

“Labda Ronaldo angeweza kutoa sehemu ya mshahara wake kwa klabu ili waweze kumiliki wachezaji zaidi. Sijawahi kusikia kitu cha kipuuzi kama hiki maishani mwangu, ni ubinafsi wa kupindukia.” amesema Murphy

Ronaldo aliingia Al-Nassr mwaka 2022 na mkataba wake wa sasa unaisha 2027, lakini bado hajasaidia timu yake kushinda taji kubwa.

Taarifa mpya kutoka Ureno zinaonyesha kuwa Ronaldo anaweza kufikiria kuondoka klabuni hapo majira ya kiangazi hii.