Baadhi ya wakazi wa jimbo la Busanda mkoani Geita wameiomba serikali kupitia mbunge wa jimbo hilo kuendelea kuwaboreshea huduma za afya katika maeneo yao kwani idadi ya watu inazidi kuongezeka na uhitaji wa huduma za afya ususani kwa akina mama wajawazito ni mkubwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa jimbo hilo wamebainisha kuwa licha ya kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya ujenzi wa zahanati na vituo vya afya katika jimbo hilo bado kuna uhitaji wa huduma za upasuaji kufanyika katika vituo vya afya vilivyopo katika jimbo hilo.
Mganga mfawidhi kituo cha Afya Bukoli Simoni Mlyabuso amesema matarajio yao baada ya hapa ni kuhakikisha wanafanya maboresho ya kituo hicho pamoja na ujenzi wa Chumba cha kuifadhia maiti.
