Mmoja wa Viongozi wa MVIWATA Akizungumza katika moja ya Makongamo ya Wanachama wa vikundi vya Wakulima wadogowadogo.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari katika kata ya Dosidosi na Magungu Wilayani Kiteto baadhi ya viongozi wa vikundi hivyo wameeleza kuwa mradi huo umeleta mafanikio makubwa na kubadilisha maisha ya wakulima wadogo kutoka na kuongeza kipato chao.
Mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Alliance for Gree Revolution in Africa AGRA na kusimamiwa na MVIWATA, umemaliza tatizo hilo kwa kuwaunganisha wakulima hao na masoko mbalimbali kwa kusudio la kuboresha biashara zao na kuepuka ulanguzi.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi huo kutoka MVIWATA, Geofrey Kabuka amesema mradio huo umekuja kufuatia utafiti uliofanyika katika wilaya mbalimbali nchini na kubaini pamoja na wakulima kuzalisha kwa kiwango cha chini lakini wamekuwa wakinyonywa na walanguzi na kuuza nafaka kwa bei ya chini.