
Akimshukuru Trump kwa mazungumzo yenye tija siku ya Jumanne, Zelensky alidai kuwa Moscow ilikuwa suala nyeti haswa kabla ya siku ya ukomo ya Urusi kusitisha vita iliyowekwa na Rais Donald Trump.
Trump aliwahi kusema kuwa ikiwa Urusi itashindwa kusitisha mapigano na Ukraine ifikapo Ijumaa hii, itakabiliwa na vikwazo vikali au kushuhudiwa kwa vikwazo vingine dhidi ya wale wote wanaofanya biashara nayo.
Aidha, siku ya Jumatatu Rais Volodymyr Zelensky alisema kwamba wanajeshi wa Ukraine kaskazini-mashariki mwa Ukraine walikuwa wakipambana na "mamluki" wa kigeni kutoka nchi mbalimbali zikiwemo China, Pakistan na sehemu za Afrika, na kuapa kulipiza kisasi.
Zelensky aliwahi kuishutumu Moscow kwa kusajili wapiganaji wa China kwa ajili ya juhudi zake za vita dhidi ya Ukraine, mashtaka ambayo Beijing ilikanusha, wakati Korea Kaskazini pia imetoa maelfu ya wanajeshi wake kupigana katika eneo la Kursk nchini Urusi.
Witkoff atakuwa mjini Moscow na anatarajiwa kukutana na Vladimir Putin.