
Wachezaji wa The Blues walifanya mazoezi katika uwanja wa Subaru Park nyumbani kwa klabu ya Philadelphia Union ya inayoshiriki ligi kuu nchini Marekani hali ya hewa ikiwa ni nyuzi joto 37 unyevunyevu wa 45%.
Chelsea wanashika nafasi ya 2 katika kundi D sawa na Esperance waliopo nafasi ya 3 ushindi wowote katika mchezo huo au sare utawavusha katika hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la Dunia ya vilabu inayoendelea nchini Marekani.