Monday , 19th May , 2025

Msanii Chino Kidd amefunguka kuwa bado yupo chini ya mwamvuli wa Bad Nation yake msanii Marioo na kusema kuwa kuwa chini yake haimaanishi kunamfanya kuwa msanii mdogo au mkubwa kwasababu kinachofanya msanii kuwa mkubwa ni kazi na sio mwamvuli

Pichani Marioo Na Chino Kidd

Akipiga story na kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Televisino Chino Kidd Amesema....."Wote tupo chini ya Bad Nation na hamna mtu ambaye anajikuzisha mfano kaka yangu Diamond ametokea Sharobaro lakini sasa hivi Diamond ni mkubwa kuliko Sharobaro kwahiyo kukua ni wewe mwenyewe unavyopambana''

"Mwamvuli haukufanyi uwe chini zaidi mwamvuli unakubariki hivyo unapaswa kuuheshimu lakini pia usijijaze kuwa kukaa hapa unakuwa mdogo udogo/ukubwa ni wewe unavyofanya kazi'' Amesema Chino Kidd