Tuesday , 22nd Apr , 2025

Licha ya 5ive ya Davido kupokelewa kwa kishindo na mashabiki duniani kote, bado hajafanikiwa kufuta rekodi iliyowekwa na Wizkid kupitia albamu yake ya Morayo kwenye Spotify. Albamu hiyo ya Wizkid inaendelea kushikilia rekodi ya kuwa na streams nyingi zaidi kwa siku moja Nigeria

Pichani ni Davido na Wizkid

Kilichovutia zaidi ni athari chanya ya Davido kwa wasanii wenzake aliowashirikisha kwenye albamu hiyo. Wimbo wake "With You" akimshirikisha Omah Lay umepanda kwa kasi kwenye chati ya Global Shazam, ukitua nafasi ya 38 baada ya kuruka nafasi 65 ikiwa ni hatua kubwa kimataifa.

Athari hiyo pia imeonekana kwenye rekodi binafsi za wasanii aliowapa nafasi kwenye kazi yake, Omah Lay amevunja rekodi yake kwa kupata streams milioni 3.42 ndani ya siku moja.

Shenseea naye amefikia milioni 2.4 rekodi yake kubwa zaidi hadi sasa.

Victony hakubaki nyuma, akiweka alama ya streams milioni 2.08, kiwango chake kikubwa zaidi katika historia ya Spotify.