Friday , 11th Apr , 2025

Dimitri Payet anaripotiwa kuchunguzwa na polisi nchini Brazili baada ya kushutumiwa kwa 'unyanyasaji wa kimwili na kisaikolojia' dhidi ya aliyekuwa mpenzi wake Larissa Ferrari  wakati wa mapenzi yao ya miezi saba.

Dimitri Payet na mpenzi wake Larissa Ferrari

Nyota huyo wa zamani wa West Ham anadaiwa kumlazimisha Larissa Ferrari mwenye umri wa miaka 28, kunywa mkojo wake na kulamba sakafu pamoja na kumsukuma na kumkanyaga.

Nyota huyo wa zamani wa West Ham na kiungo wa kikosi cha Vasco da Gama, anaripotiwa kuwa chini ya uchunguzi wa polisi mjini Rio de Janeiro kutokana na changamoto hiyo.

Kwa mujibu wa AFP ripoti ya polisi ya Machi 29, mwanamke huyo alisema "Nilishambuliwa na kuachiwa alama kwenye mwili wangu kwa kupigwa na kusukumwa kisha kudhulumiwa kimwili, kimaadili, kisaikolojia na kingono.

Mwezi Desemba, tuligombana akaniomba uthibitisho wa mapenzi, ambao ulikuwa na udhalilishaji. Nilirekodi video nikinywa mkojo wangu, kunywa maji kwenye bakuli la choo na kulamba sakafu,"