Monday , 24th Mar , 2025

Miongoni mwa mahojiano ambayo aliyafanya beki wa zamani wa Manchester United Patrice Evra ni kuhusu mabadiliko ya soka duniani chini ya Kocha Pep Guardiola kuwa ameua Soka kutokana na falsafa yake ya ufundishaji.

Pep Guardiola na Patrick Evra

Evra anaamini mpira wa kisasa umemfanya mchezaji asiwe huru zaidi ya kufuata zaidi maelekezo ya kocha tofauti na zamani.

Evra anasema “Guardiola ni moja ya Makocha bora lakini ameua Soka. Sisemi hivi kisa utani wa jadi Man United na Man City. Hapana! Kwa sababu kwa sasa tuna wachezaji maroboti. Kwenye Akademi, kila mtu anataka kucheza kama Guardiola. Kipa lazima awe na sifa za number 10. Beki wa kati anapaswa kufanya tackle, acheze vichwa, vitu kama hivyo.”

“Hii Tiki-taka ni Guardiola pekee anayeweza kuifanya. Kwanini kila mtu anamuiga Guardiola? Hatuna tena ubunifu; tumekosa fikra mpya.

Huwezi kuona mchezaji kama Ronaldinho tena au Hazard au chochote kile. Kwa sababu wakati kijana akiwa mdogo, wale makocha watamwambia, usipopiga pasi, nitakuweka benchi.”-Patrice Evra kwenye podcast na Rio Ferdinand