
Arne Slot - Kocha wa Klabu ya Liverpool
The Reds wameongoza hatua ya ligi ya Ligi ya Mabingwa wakiwa wameshinda mechi 7 kati ya 8 na kwa sasa wanaongoza Ligi Kuu ya Uingereza kwa tofauti ya alama 13, hii leo wako Ufaransa kupambana na PSG katika mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora.
"Ni pongezi nzuri kupata lakini timu bora zaidi barani Ulaya inapaswa kushinda Ligi ya Mabingwa lakini sisi tuko mbali na hilo, tunaanza na mchezo mgumu sana dhidi ya PSG,kwa upande wangu ukiniuliza timu bora nitajibu Madrid ambao wamebeba kombe hili msimu uliopita "
Arne Slot akijibu kauli ya kocha mkuu wa PSG Luis Enrique aliyesema Liverpool ni timu bora.