Monday , 25th Nov , 2024

Linaweza kuwa swali lenye majibu mengi ndani yake kwa sababu kila mtu yuko na namna ya tofauti ambayo anatafsiri utajiri wa fedha na mali.

Lakini kwa wewe Mtanzania huenda ulishawahi kuwaza hapa nikipata Milioni 50 tu, nishakuwa tajiri

Mambo ni tofauti kidogo kwa wenzetu, kwani utafiti uliyofanywa na kampuni ya Charles Schwab kutokea nchini Marekani umekuja na majibu ya kwamba, kwa mwananchi wa Taifa la Marekani ili ajihesabu kama ni tajiri basi anahitaji kuwa na kiasi cha pesa zaidi ya Bilioni 5

Na majibu haya ya tafiti yako kwa wastani, kwani kuna baadhi ya majimbo kama vile San Francisco wakazi wa maeneo hayo tafsiri ya mtu tajiri kwao ni lazima awe na utajiri wa kuanzia Bilioni 11

Kwenye hili la utajiri ipo hoja ya vizazi ambayo haipewe mashiko sana, ikisema kwamba kila kizazi kina kiwango chake cha kutafsiri utajiri.