Miguel Gamondi alijiunga na Yanga SC Juni 2023 kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwalimu wa timu hiyo ya Wananchi Mtunisia Nesreddine Nabi ambaye alitimkia AS FAR Rabat ya nchini Morocco.Gamondi anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kufundisha mpira wa kushambulia na burudani kutokana na asili yake ya America ya Kusini kucheza mpira huku ukiwa na tabasamu mdomoni mwako.Ameiongoza timu ya Wanajangwani kushinda Kombe la Shirikisho Tanzania, Kombe la Ligi kuu Tanzania bara pamoja na kucheza hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika.
Klabu ya Yanga imetangaza kuachana na Kocha wake Miguel Gamondi hii leo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na timu hiyo kupitia ukurasa rasmi wa Instagram klabu hiyo.Klabu hiyo pia imesitisha mkataba wa aliyekuwa msaidizi wa Muargentina huyo Moussa Ndaw.
Sababu zinazosemekana kumfukuzisha kazi Ganondi kupoteza uwezo wa kushawishi wachezaji kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ( Dressin Room), kushindwa kuzibiti nidhamu za Wachezaji pamoja na kushuka kwa viwango vya wachezaji ndani ya kikosi hiko.
Kikosi cha mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara kimepoteza michezo miwili mfululizo ligi kuu Tanzania bara kabla ya mapumziko ya kupisha michezo ya kufuzu michuano ya AFCON 2025 nchini Morocco.Yanga SC ilipoteza michezo dhidi ya Azam FC kwa goli 1-0 na Tabora United 3-1.
Kuna taarifa ambazo si rasmi ambazo zinazagaa nchini kwa sasa ni kuhusiana na ujio wa Kocha mpya Sead Ramović aliyekuwa akihudumu kikosi cha TS Galaxy ya Afrika ya Kusini.Ujio wa Kocha huyo raia wa Ujerumani ukadhibitisha zile taarifa za kusadidkika za kufukuzwa kwa Gamondi.
Miguel Gamondi alijiunga na Yanga SC Juni 2023 kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwalimu wa timu hiyo ya Wananchi Mtunisia Nesreddine Nabi ambaye alitimkia AS FAR Rabat ya nchini Morocco.Gamondi anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kufundisha mpira wa kushambulia na burudani kutokana na asili yake ya America ya Kusini kucheza mpira huku ukiwa na tabasamu mdomoni mwako.Ameiongoza timu ya Wanajangwani kushinda Kombe la Shirikisho Tanzania, Kombe la Ligi kuu Tanzania bara pamoja na kucheza hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika.
Atakumbukwa zaidi kuwa ndiye Kocha pekee ambaye kafanikiwa kuutawala mchezo wa Dabi ya Kariakoo kwa kuifunga timu Mtani wake wa jadi Simba SC kwenye michezo minne mfululizo hakuna Kocha amewahi kufikisha rekodi hiyo.
Yanga SC inaanza upya chini ya Kocha mpya ili kufikia malengo iliyojiwekea kama taasisi kutetea ubingwa wake wa ligi kuu, ubingwa wake wa kombe la shirikisho Tanzania pamoja na kufanya vizuri mashindano ya klabu bingwa Afrika.Michezo yake ijayo baada ya mapumziko ya michezo ya timu za taifa kukamilika itakuwa dhidi ya Al -Hilal Omdurman tarehe 26 Novemba 2024 na Namungo FC tarehe 30 Novemba 2024.