Saturday , 9th Nov , 2024

Katibu Mkuu, UTUMISHI, Juma Mkomi amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan ( JICA),  Ara Hitoshi kuhusu kuimarisha ushirikiano baina ya JICA na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora. 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI Juma Mkomi akisalimiana na Mwakilishi wa ( JICA), Ara Hitoshi.

Kikao hicho kimefanyika  leo  katika Ofisi zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma Miongoni mwa masuala waliyojadili ni pamoja na kutoa fursa za mafunzo kwa watumishi pamoja na maombi  ya vibali vya ajira  kwa raia wa kutoka Japan wanaokuja kufanya kazi nchini katika miradi ya Serikali katika Utumishi wa Umma  ambapo fursa  hiyo huwasaidia Wazawa kubaki na ujuzi  unaoweza kutumika hata baada ya miradi ya maendeleo kukamilika 

Aidha, viongozi hao wamepongeza juhudi za ushirikiano wa nchi hizo mbili unaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Japan,  Shigeru Ishiba.

Akizungumza kwenye kikao hicho Katibu Mkuu Mkomi  ameishukuru JICA kwa kuendelea kutoa  ufadhili masomo wa elimu ya juu kwa Watanzania hususani   watumishi wa umma huku akisisitiza kuwa   ushirikiano baina pande mbili ni  wa kihistoria na utaendelea kuimarika   wakati wote katika masuala ya elimu na utumishi wa umma