Tuesday , 22nd Oct , 2024

Aishi Manula amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kitakachocheza mchezo wa kufuzu michuano ya CHAN dhidi ya timu ya taifa ya Sudan ugenini Oktoba 27, 2024 na mchezo wa marudiano utachezwa Jijini Dar es salaam Benjamini Mkapa Novemba 3, 2024.

Aishi Manula mara ya mwisho kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania ilikua mwezi Machi 2024.Kumekua na mjadala mkubwa kwa Wapenzi na Wadau wa soka nchini Tanzania kuhusiana na nafasi ya Golikipa huyo wa timu ya Simba kwenye kikosi cha Stars. Manula hana Wakati mzuri kwenye klabu yake ya Simba ameondolewa kwenye nafasi yake ya kuwa golikipa namba moja baada ya kuumia kwa muda mrefu na aliporejea uwanjani kwenye mchezo wa Dabi ya Kariakoo alifanya makosa yaliyochangia kupoteza mchezo kwa goli 5-1.

Mlinda mlango wa Simba SC AishI Salum Manula amejumuishwa katika kikosi cha Taifa Stars kitakachocheza mechi za kuwania kufuzu CHAN 2025 baada ya kukaa nje ya kikosi hiko tangu Machi 2024 kutokana na kukosa nafasi ya kucheza kwenye kikosi chake cha Simba SC.

Tanzania itaikabili Sudan ugenini Octoba 27 2024 huku mechi ya marudiano itapigwa Benjamini Mkapa Novemba 3 2024

Kikosi hiko chenye  wachezaji 24 kitakuwa chini ya kocha Bakari Shime ambaye pia ni kocha mkuu wa timu za taifa za wanawake   kimejumuisha wachezaji 11 kutoka katika kikosi cha Tanzania Wachezaji wenye umri chini ya miaka 20  ‘Ngorongoro Heroes’ ambacho kimetoka kubeba ubingwa wa CECAFA kwenye mchezo wa fainali uiliochezwa Dimba la KMC siku ya Jumapili  Oktoba 20, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Kumeibuka mijadala kuhusiana na nani anatakiwa kusimama kwenye goli la timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kutokana na makosa yanayofanywa na Magolikipa wanaoitwa badala ya Aishi Manula. Manula hana wakati mzuri kwenye kikosi chake cha Simba SC kwa sasa kutokana na kupoteza nafasi yake ya kusimama kama golikipa namba moja kwa Ayoub Lakred na Moussa Cammara.

Manula anauzoefu wa kucheza michezo mingi ya taifa Stars na klabu yake ya Wekundu wa Msimbanzi kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika pamoja na ile ya shirikisho. Amechangia kwa kiasi kikubwa kwenye mafanikio ya kikosi cha Simba kipindi chote cha utawala wao soka la Tanzania kwa miaka minne mfululizo.

Nyota huyo wa zamani wa klanu ya Azam anatarajiwa kuonyesha kiwango kikubwa kwenye michezo dhidi ya Sudan ili kurudisha imani kwa Kocha Hemed Morocco ili aweze kumjumuisha kwenye kikosi cha Stars kitakocheza michezo ya kufa au kupona kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Guinea na Ethiopia.