Barani Ulaya kwa sasa Wachezaji Wanaongoza kwa ufungaji wa magoli kwenye ligi kuu Tano kubwa ni Washambuliaji wa kati. Mabadiliko ya Sayansi ya mpira wa miguu imepelekea kupoteza baadhi ya Wachezaji ambao walisifika kwa kutimiza majukumu yao yaliyokuwa yanawaweka ndani ya uwanja.Mabadiliko wa kiucheza na mifumo mipya kwenye mpira wa miguu imepelekea kuibuka kwa Wachezaji wa pembeni yao Mawinga kutumika kama Washambuliaji wa kati na kumfanya namba Tisa ili aweze kucheza awe na sifa ya kuchezesha wengine kama kiungo wa kutokea juu yaani inside Forward. Harry Kane, Karim Benzema na Robert Firmino ni mfano sahihi wa Washambuliaji wa kati wenye uwezo wa kuchezesha wengine ndani ya uwanja.
Kwenye ligi Tatu kubwa barani Ulaya msimu huu wa 2024-2025 wanaoongoza kwenye chati ya Wafungaji bora ni Washambuliaji wa kati asilia yaani namba 9. Mabadiliko ya Sayansi ya mpira na mifumo sambamba na falsafa za Walimu zikapelekea Washambuliaji wa kati kufutika na nafasi zao kuchukuliwa na Wachezaji wa pembeni wenye uwezo wa kufunga ( Goal scoring Wingers) Mfano alisi wa kundi hili la Wachezaji ni Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Frank Ribbery, Arjen Robben, Mohamed Salah, Sadio Mane na Eden Hazard.
Uwepo wa Makocha kama Pep Josep Guardiola na Jurgen Kloop kulibadili baadhi ya majukumu ya Washambuliaji wa kati ili kuweza kutengeneza timu zao kulingana na sifa za Wacchezaji ambao wanapatikana kwenye timu zao. Pep aliaanza kumtumia Messi kama namba 9 wa uongo alipokuwa anaifundisha klanu ya Barcelona na kuifanya Barca kucheza bila uwepo wa Mshambuliaji wa kati asilia.
Muhispania huyo pia alimtumia Mario Gotze alipokuwa akiifundisha Bayern Munchen ya Ujerumani kipindi ambacho timu hiyo ilikuwa na Robert Lewandoski kama Mshambuliaji wa kati, huku Frank Ribbery na Arjen Robben wakitumika kama Washambulizi wa kutokea pembeni.
Barani Ulaya tunashuhudia kurudi kwa Washambuliaji wa kati na Wanatumiwa kwenye maeneo yao ya asili na Wameanza kuturudisha kwenye ladha ya mpira kama ilivyokuwa awali. Ligi ya Ujerumani anayeongoza kwa kufunga Harry Kane mshambuliaji wa kati, Robbert Lewandoskianaongoza kwenye La liga na Uingereza anayeongoza kwa ufungaji ni Erling Haaland.
Muda mrefu Dunia haikushudia vita ya Washambuliaji wa kati asilia kugombania kiatu cha ufungaji bora barani Ulaya. Erling Haaland ameshafunga goli 10 EPL, Harry Kane ameshafunga goli 8 Ujerumani na Robbert Lewandoski amefunga goli 12 kwenye michezo 10.
Ushindani wa mbio za ufungaji bora barani Ulaya unategemewa kuwa mkubwa msimu huu wa 2024-2025 kutokana na uwepo wa Washambuliaji wa kati wenye uwezo mkubwa kufunga magoli.
Uwepo wa Wachezaji wa eneo la namba 9 kwenye timu ambazo zinauwezo wa kutengeneza nafasi wa upatikanaji wa kufunga kunaweza kurudisha hadhi ya Washambuliaji wa kati na kufanya Ulimwengu wa mpira kuanza kuzalisha Washambuliaji wa kati au namba 9 ambao kwa kiasi kikubwa magoli wanayofunga huwapa timu zao ubingwa wa ligi wanazoshiriki pamoja na makombe mengine mbalimbali.