Thursday , 17th Oct , 2024

Google kwa sasa wametambulisha feature mpya ambayo itamsaidia mtumiaji wake kupata bei za safari za ndege kwa bei nafuu zaidi.

 

Huenda ukawa ni mmoja ya wale ambao wanatazamia kufanya booking ya ndege kwa ajili ya sikukuu zinazokuja miezi ya mbele kama vile christmas na mwaka mpya.

Lakini mpaka sasa hujafahamu ni wapi unaweza kupata tiketi ya safari yako kwa bei nafuu zaidi, Google wametambulisha feature mpya ambayo inafahamika kama ''Google Flights'' ikiwa na kazi maalumu kukusaidia kupata tiketi za ndege kwenye sehemu unayokwenda kwa bei nafuu.

Kutambulishwa kwa Google Flights kwenye kipindi hiki, imeonekana kuwa mkombozi mkubwa kwa mujibu wa tafiti za awali kwani ni kipindi ambacho watu wengi wanakaribia mapumziko ya mwaka.

Namna ya kupata sasa punguzo la bei kwenye safari za ndege kupitia Google Flights

Ingia kwenye google kama mtumiaji wa kawaida, kisha kwenye machaguo ya juu kabisa utakutana na ongezeko jipya limeandikwa flights ikiwa kama hupati chaguo hili basi utaandika Google Flights kwenye google alafu utaandika sehemu uliyopo na unayotamani kwenda, siku na tarehe husika kisha itakuja orodha ya ndege zinazopatikana kwenye eneo lako na bei husika

Kwa sasa hutotapata kuona machaguo hayo lakini kwa wiki mbili zijazo itapatikana kwa watu wote ikiwa na chaguo la Best na Cheapest price ndani yake na ndiyo hapo sasa utaweza kupata tiketi kwa bei punguzo zaidi bila uwepo wa dalali.

Kwa mujibu wa takwimu za Google kwa mwezi uliyopita, safari za ndege ambazo zilikuwa ni za moja kwa moja bila kusimama na kubadili ndege ziligharimu asilimia 25 zaidi ukilinganisha na zile zilizohusishwa kusimama kwenye vituo na kubadili ndege

Na siku za Jumatatu, jumanne na jumatano ndiyo zilikuwa siku zenye unafuu zaidi kwa asilimia 13 kwenye bei za tiketi kwenye ndege ukilinganisha na siku nyingine.