“Wapinzani wetu (Al Ahly Tripoli) wameshaingia nchini na mkwala mzito, wamekodi mabaunsa wengi kwelikweli kwa kutambua ugumu ulipo. Sisi ni wengi kuliko mabaunsa wao, tunapaswa kwenda kuwaonyesha kwamba pamoja na wote mliokodi hamuwezi kufanya lolote mbele ya Nguvu Moja ya Simba Sports Club.” Ahmed Ally, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC
Septemba 22 2024 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa wakiwa na kumbukumbu ya kutoshana nguvu kwenye mchezo uliopita wakiwa ugenini kwa ubao kusoma 0-0