Wednesday , 18th Sep , 2024

Mshambuliaji wa England Harry Kane amefunga magoli 4 katika ushindi wa mabao 9-2 walioupata jana Bayern Munich kwenye michuano ya UCL dhidi ya Dinamo Zagreb na kumfanya afikishe mabao 53 kwenye mechi 50 ndani ya kikosi hiko

Magoli hayo pia yamemfanya Kane kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Uingereza  kufunga goli 4 kwenye mechi moja ya UCL na ni Muingereza wa kwanza kufunga goli 4 kwenye timu nje  ya England

Magoli hayo pia yamemfanya Kane awe mfungaji bora wa muda wote kwa wachezaji wa Uingereza kwenye michuano ya UEFA  akiwa na magoli  33 akimpita wayne Rooney mwenye magoli 30 

Je ataweza kuifikia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote UCL Cristiano Ronaldo mwenye magoli 140?