Tuesday , 20th Aug , 2024

Timu ya Kriketi ya Tanzania imetamba kufanya vyema kwenye shindano la kuwania kufuzu kushiriki kombe la Dunia kwa mchezo wa Kriketi yanayotarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Septemba 18,2024 katika viwanja viwili vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Gymkhana Jijini Dar es Salaam

Wakizungumza kwenye mazungumzo maalum  na EATV,Nyota hao wa timu ya Tanzania ambao wameshaingia kambini kujiandaa na shindano hilo wametamba kuibuka kwenye nafasi mbili za kufuzu kati ya timu 6 ambazo zinasaka nafasi kwenda kwenye Division 1 ya kufuzu kombe la Kriketi ndani ya mwaka huu.

 “Mashindano  yapo katika hatua ya DIvision 2 na iwapo tukifanya vizuri tunakwenda Division 1 na tunakuwa tumeshakata tiketi ya kushiriki mashindano hayo imekuwa ni ndoto yetu kufanya vizuri na kwenda kushiriki “wamesema wachezaji .

Hili linakuwa shindano la pili la Kriketi kuandaliwa nchini Tanzania ndani ya mwaka 2024 ambapo shindano la kufuzu kombe la Dunia U19 litakalofanyika nchini Sri Lanka ilifanyika Jijini Dar es Salaam kusaka nafasi ya kwenda Division 1 kufuzu ndani ya michuano hiyo.