Washtakiwa wa ubakaji na ulawiti
Akizungumza mahakamani hapo hii leo Agosti 19, 2024 Renatus Mkude ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mashtaka makao makuu Dodoma, amesema mashtaka yanayowakabili ni pamoja na kubaka kwa kundi na shtaka lingine ni la kumuingilia huyo binti kinyume na maumbile.
"Wamesomewa mashtaka hayo na wamekana, tutaendelea na utaratibu zingine za usikilizaji lakini lingine lililofanyika kwa mujibu wa sheria ni kumlinda huyo binti aliyefanyiwa ukatili na kama ambavyo imeonekana katikati ya mashtaka jina lake halijatajwa pale," amesema Mkurugenzi Msaidizi