Wednesday , 7th Aug , 2024

Timu ya Taifa ya Riadha itakayoiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olimpiki Paris 2024, imeondoka alfajiri ya leo Agosti 07, 2024 kuelekea Paris, nchini Ufaransa.

Timu hiyo inayoundwa na wachezaji wanne na kocha mmoja, wanariadha wote ni wa mbio ndefu (Marathon) na wanatarajia kukimbia tarehe 10 Agosti, 2024 (Wanaume) na Wanawake watakimbia tarehe 11 Agosti, 2024 ambapo itakuwa ndiyo mwisho wa muhula wa 33 wa Mashindano ya Olimpiki kwa mwaka huu.

Wanariadha hao ni Gabriel Geay, Jackline Sakilu, Magdalena Shauri, Alphonce Simbu(Nahodha) na Anthony Mwingereza (kocha).