Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kwela, Deus Sangu
na watoto kufanya kazi za kujitolea huku akionya watendaji watakaozembea kusimamia suala hilo hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao
Mhe. Sangu ametoa kauli hiyo leo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Lusaka kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika kwenye vijiji vya Lowe, Lusaka, Kizumbi na Kamnyazya vilivyopo Jimbo la Kwela , Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo.
Amezitaja kazi hizo za kujitolea ambazo huratibiwa na TASAF kuwa ni ulimaji wa barabara pamoja na uchimbuaji wa mitaro ya barabara
Amesema kundi hilo lisisumbuliwe kufanya kazi hizo kwani sio sawa kutokana na hali zao.
Katika hatua nyingine Mhe. Sangu amezitaka kaya zinazonufaika na mpango wa TASAF kuhakikisha kama zina wanafunzi waliohitimu kidato cha sita na wanatarajia kujiunga chuo kikuu wawasilishe majina yao katika ofisi za Halmashauri zao ili waweze kupata kipaumbele cha kupata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu utakaowawezesha kuendelea na masomo ya chuo kikuu kwani bodi hiyo imeingia mkataba na TASAF.
Amesema lengo la TASAF kuingia mkataba na Bodi ya Mikopo wa Elimu ya Juu ni kuhakikisha watoto wanaotoka katika kaya maskini hawakosi mkopo ili kuhakikisha wanafaulu ili badae waweze kurudi kwa ajili ya kuzikomboa Kaya zao kwenye lindi la umaskini.