Wednesday , 24th Jul , 2024

Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) limekabidhi vifaa vya michezo katika kambi ya timu ya Taifa ya riadha inayoji-andaa kushiriki Michezo ya Olimpiki kama sehemu ya kukiongezea nguvu kikosi hicho.

Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji wanne wa mara-thoni ya mbio ndefu za kilomita 42 na wamebeba juku-mu la kwenda kuandika historia ya kuleta tena medali baada ya kupita zaidi ya miaka 40.

Mara ya mwisho medali hizo zililetwa na wanariadha Su-leiman Nyambui aliyeliletea Taifa medali ya fedha mbio za mita 5000 na Filbert Bayi mita 3000 kwenye Olimpiki za Moscow urusi mwaka 1980.

Akizungumza wakati wa kugawa vifaa hivyo katika kambi ya timu hiyo iliyoko Sakina, jijini hapa, Mjumbe wa RT, Al-fredo Shahanga amesema anaamini itawaongezea morali na watarudi na medali.

Amesema vifaa hivyo ni tisheti, fulana, traki suti, viatu na jaketi watakazovaa wakati wa mazoezi, kambini na kwenye michezo hiyo.

“Sisi kama RT tunawaombea mafanikio wachezaji wetu ambao wamefikisha viwango vya kutuwakilisha Olimpiki," amesema Shahanga.

Nahodha wa timu hiyo, Alphonce Simbu ameipongeza RT kwa kutambua umuhimu wao na kuamua kuongeza nguvu katika vifaa vya michezo ambavyo vitawasaidia kushinda na kurudi na medali.

“Siku za nyuma tulikuwa hatuna kampuni ambayo ina-beba alama kwa ajili ya Tanzania lakini kwa sasa tuna-washukuru RT kwa juhudi kubwa ambazo wamefanya na kupata kampuni ambayo imetuletea vifaa hivi," amesema Simbu.