Monday , 22nd Jul , 2024

Wakulima wa pamba kutoka mitaa Kilulu na Mwanzimbila iliyopo kata ya Bunamhala halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu wamemlalamikia mtendaji wa mtaa kugawa dawa za kuulia wadudu usiku hali inayopelekea

wasiokuwa wakulima kupokea dawa hizo hatua inayopelekea baadhi ya wakulima kukosa dawa.

Wakulima hao wamesema hali hiyo inawasababishia kushuka kwa kiwango cha uzalishaji kutokana na mazao yao kushambuliwa na wadudu.

"Mtendaji wa mtaa wa Mwazimbila anagawa dawa kuanzia saa 9 au saa 11 alafu anamaliza saa 12 na wanaopewa dawa si wadau wa pamba tukifika walimaji wa pamba mnaambiwa kwamba dawa imeshaisha dawa tunagawiwa kinyume baba"MADUHU MASANJA,Mkazi wa Bunamhala.

"Unaweza ukaja asubuhi hapa ukaambulia huna dawa lakini viongozi waliopo mahali hapa jioni unakutana na watu wana dawa wengine ambao mmesambaa nao wakati mwingine mpaka pamba yetu inamalizwa kwasababu viongozi ambao tunawaweka sisi wenyewe madarakani dawa inaelekea ambayo hata wakulima sio wakulima wa pamba" JUMA HOSEA,Mkazi Bunamhala.

Afisa ugani wa kata hiyo Paul Mahalu anakiri uwepo wa changamoto hiyo.

"Utaratibu sumu haziwezi kugawiwa mida hiyo ya usiku dawa zinagawiwa mida ya saa mbili kwa wakulima wote wanaolima pamba wamealikwa kwaajili ya kugawa hizo pembejeo kiongozi yeyote wa serikali ambaye anagawa sumu mida ya usiku huyo ana lengo tofauti na maelekezo ya serikali ambayo yametolewa eneo hili la kilulu pamoja na Mwanzimbila kumekuwa na malalamiko mengi sana ambayo wananchi wa eneo hilo walikuwa wanatoa na tayari tulimuita kwenye ofisi ya kilimo akapewa onyo akasema hatarudia lakini changamoto hiyo iliendelea kujitokeza na wakulima walienda mbali zaidi walipiga simu kwenye taasisi nyingine hiyo taasisi walifika eneo hilo bahati nzuri walikuta kuna ukiukwaji wa ugawaji wa hizo pembejeo na walichukua hatua na mpaka sasa hivi mkurugenzi wangu ameshachukua hatua ya kidogo kazi kwaajili ya taasisi hiyo iweze kuendelea kufanya shughuli yake" PAUL MAHALU,Afisa ugani kata ya Bunamhala.

Serikali tayari imechukua hatua dhidi ya mtendaji huyo.

" Mkurugenzi huyu mtu ambaye amepewa jina na wananchi hapa mpenda pesa mimi sitaki kutaja jina lake la kwanza wenyewe wanamuita mpenda pesa na inaonekana hapa kwenye mtaa huu wamemlalamikia lakini mtaa ambao aliuchagua ndio aliokuwa anaufanyia kazi wamemlalamikia na anadaiwa na wananchi wengi moja vyombo vya usalama vinavyohusika vyombo vya uchunguzi vimchunguze wakati vinamchunguza nimeambiwa mmeshamsimamisha si ndio...ndio...lakini wakati amesimama hata kama itaonekana vinginevyo mtafutie eneo lingine hawa wananchi wamemkataa ...mnamtaka arudi ama...hamna...mkiona wanamuita tena mpenda pesa hii sio sifa nzuri na ndio maana na wewe umechukua hatua kwamba malalamiko ya wananchi dhidi yake yalikuwa makubwa mno hiyo sio sifa ya mtumishi wa umma"SIMON SIMALENGA,Mkuu wa wilaya ya Bariadi.