Mshukiwa huyo ametajwa kuwa Collins Jomaisi Khalisia ambaye sasa anazuiliwa kwa uchunguzi zaidi.Mkurugenzi wa idara ya upelelezi Amin Mohammed amesema mshukiwa amekiri kuwaua watu 42 kati ya mwaka wa 2022 na Julai tarehe 11 mwaka huu. Amin pia amesema mshukiwa alikiri kutekeleza mauaji ya mke wake.
Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 33 alikamatwa katika klabu moja ya burudani katika mtaa wa Kayole viungani mwa jiji la Nairobo na alipatikana akiwa na kadi nyingi za simu.
Anashukiwa kuwaua waathiriwa wake kuifunga miili yao katika mifuko ya plastiki na kisha kuitupa katika jalala la Kware.