ameachiwa huru baada ya kulipa faini Kwa fedha alizochangiwa na wananchi.
Kijana Shadrack alipewa hukumu hiyo Julai 4, 2024 baada ya kupatikana na hatia ya kuchapisha taarifa uongo mitandaoni, kosa alilolifanya June 22 akiwa katika Kijiji Cha Ntokela na huku akijirekodi video akiwa anachoma picha inayomuonesha Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ilimhukumu Chaula ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Ntokela mkoani Mbeya, kutumikia kifungo hicho, baada ya kukutwa na hatia ya kuchoma picha ya Rais