Baadhi ya Wananchi Wakishudia Ajali Iliyomgonga Mwendesha Bodaboda
Watu watatu wamenusurika kifo baada gari namba T 422 AKF yenye tela T303 APW Scania lilokuwa nimebeba shehena ya mchele likitokea Jijini Dar-es-salaam kuelekea nchini ya Zambia baada ya kumgonga mwendesha bodaboda na badaye kuacha njia na kupinduka katika eneo Mbembela kata ya Nzovwe jijini Mbeya barabara kuu ya Mbeya -Tunduma.
Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Abdi Isango amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba watu watatu wamejeuriwa na wote wapo Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya wakiendelea kupatiwa matibabu.