Ramadhani Wasso alikuwa ni mchezaji pekee wa kigeni aliyekuwepo kwenye kikosi cha Simba SC kilichoivua ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Afrika Zamalek ya Misri msimu 2003-04 na kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa barani Afrika .
Atakumbukwa kwa kisa chake cha msimu 2004-05 kugoma kusaini mkataba mpya ndani ya Simba SC kwamba anaenda Ubelgiji kabla ya kutimkia ndani ya Yanga kwa msimu huo na kusaini kandarasi ya miaka 2 kwa vijana hao wa Jangwani.