Picha ya Zahara
Taarifa za kifo chake zimetolewa na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni Afrika Kusini Zizi Kodwa kupitia mitandao yake akieleza kwa masikitiko makubwa kifo cha msanii huyo.
Inaelezwa kuwa Zahara alikuwa amelazwa Hospitali wiki moja kabla, muda mfupi baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa huku chanzo cha kifo chake kikidaiwa ni maumivu makali ya mwili.
Staa huyo alitamba na nyimbo zake kama Loliwe, Destiny, Ndiza na Phendula.