Thursday , 2nd Nov , 2023

Kiungo mkata umeme wa Manchester United Casemiro amepata maumivu jana katika mchezo dhidi ya Newcastle Uinted yatakayomfanya aweze kukosa mchezo dhidi ya Fulham jumapili.

Kocha ‘Babu Kipara’ Erik ten Hag amethibitisha kuwa Casemiro alimtoa kwenye mchezo wa jana kutokana na maumivu hayo na ikumbukwe ndio alikuwa amerejea kwenye majeruhi yaliyokuwa yamemuweka nje wiki tatu.