Tuesday , 24th Oct , 2023

Bweni la Shule ya sekondari ya wasichana Marry Queens of Peace inayomilikiwa na kanisa Katholiki Jimbo la Geita limeungua kwa Moto na kuunguza baadhi ya vifaa ya wanafunzi na kusababisha majeruhi ya wanafunzi watano kwasababu ya mshituko walioupa

Jeshi la zimamoto lilifika eneo la tukio mapema na kutoa msaada wa kuokoa baadhi ya vifaa vya wanafunzi huku wanafunzi watano wakikimbizwa hospitali baada ya hali zao kuwa mbaya kutokana na mshituko walioupata

Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita Mratibu Shabani Dawa akithibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na jeshi la zimamoto linaendelea na uchunguzi.

"Kuna Bweni moja la wasichana lilikuwa linaungua katika Shule ya Marry Queen sekondari tulifika  mapema moto tukaudhibiti hakuna kifo kilichotokea lakini kuna majeruhi watano kwa ajili ya mshituko na kuna baadhi ya wanafunzi wamepoteza vitu vyao yakiwemo magodoro na nguo"