Monday , 23rd Oct , 2023

Mahakama ya juu nchini Nigeria imeanza kusikiliza kesi ya upinzani kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa Februari 2023.

  Bola Tinubu alishinda uchaguzi huo , lakini wapinzani wake wakuu , Atiku Abubakar na Peter Obi - wanataka mahakama ya juu zaidi nchini humo kubatilisha uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya Uchaguzi, ambayo iliunga mkono ushindi wa Bw Tinubu.

Changamoto ya kisheria inatishia kuongeza mvutano na kuendelea na mgawanyiko wa nchi kwenye mistari ya vyama vya siasa.

Inaweza kuchukua wiki chache kabla ya majaji saba wa jopo la Mahakama Kuu kutoa uamuzi juu ya suala hilo.

Ikiwa itaunga mkono uamuzi wa mahakama ya chini, hiyo itakuwa kufuata mfano ulioonekana katika uchaguzi uliopita katika taifa lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika ambapo matokeo ya uchaguzi wa rais hayajabatilishwa.

Hata hivyo, Bw Abubakar amesema kuwa atawasilisha ushahidi mpya mahakamani kuhusiana na mjadala wa iwapo rais amewasilisha cheti cha elimu bandia kwa tume ya uchaguzi kama ushahidi wa kustahiki kwake.