Milipuko inayoendelea kwenye kambi ya Jeshi la Polisi Mkomazi
Hayo yamesemwa leo Oktoba 20, 2023, na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) SACP Dkt Lazaro Mambosasa, wakati akifungua mafunzo ya mbinu za medani za kivita kwa kundi la Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wanafunzi eneo la Mkomazi mkoani Tanga
Dkt. Mambosasa ameongeza kuwa endapo wananchi wataona kitu chochote chenye mfanano wa chuma au kipisi cha bomba wasiokote kama chuma chakavu huku akiwaomba wananchi hao kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili wataalam wa milipuko wafike ili wavitambue kama ni vilipuzi vyenye kuleta madhara kwa binadamu.
Aidha amewataka maafisa na wakaguzi wasaidizi wanafunzi kuyapokea kikamilifu mafunzo hayo ambayo yatawaongezea mbinu za kimedani katika utendaji wa kazi za jeshi hilo katika kipindi hiki cha mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Kwa upande wake Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam DPA Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Andrew Legembo, amesema mafunzo hayo yatawaongezea uwezo wa kimedani maafisa na wakaguzi wasaidizi wanafunzi katika kukabiliana na matishio ya kiusalama katika kutekeleza majuku yao.