Monday , 16th Oct , 2023

Mwanamuziki Foby ameshea taarifa ya kuondokewa na baba yake mzazi leo Oktoba 16, 2023.

Picha ya mwanamuziki Foby

Foby ameandika ujumbe mzito kuhusu kifo hicho cha baba yake kupitia Instagram yake akiandika "Watu hawakujua, niliacha muziki kwa muda ili ukae sawa kiafya tangu April 2021 mpaka tarehe ya leo"

"Jana tumeongea mengi tu na tulipanga nikurudishe mkoa ili nirudi kwenye Game ya Music na ulikuwa unaendelea vizuri kabisa. Why hukuniambia unaicha dunia kabisa. RIP Daddy nakupenda sana".

East Africa TV na East Africa Radio tunatoa salamu za pole kwa Foby na Mungu amtie nguvu katika kipindi hiki.