
Nahodha wa TMT Isihaka Masoud amesema wamejiandaa kumaliza fainali mapema ndani ya mechi tatu za kwanza ili kuepuka gharama na usumbufu kwa mashabiki ambao watajitokeza kushuhudia mpambano wao.
"Sisi tumeshajiandaa na hatuitaji gharama zaidi kwa sababu kwenda kila siku uwanjani ni gharama ukizingatia pia tuna mambo megine ya kufanya kwa hiyo game tatu tu zitatutosha kumaliza mchezo," Nahodha wa TMT Isihaka Masoud
Kwa upande wake nahodha msaidizi wa Mchenga B Ball Stars, Amini Mkosa amesema timu yao imejiandaa kuzoa shilingi milioni kumi mapema huku akiwataka wadhamini wa michuano kuwakabidhi mapema TMT kitita chao cha milioni tatu.
"Sisi tungewashauri tu Sprite wawapatie kabisa TMT milioni tatu zao halafu watangaze kuwa Mchenga wameshinda milioni 10 kwani sisi mchezo tutaumaliza mapema sana na kama watataka tucheze 'game' tano tunawakaribisha kufanya biashara" Nahodha msaidizi wa Mchenga B Ball Stars Amini Mkosa
Mechi ya kwanza kati ya tano zitakazochezwa katika fainali ya Sprite BBall Kings 2017 itapigwa siku ya Jumapili kuanzia saa kumi jioni katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay.
Wasikilize hapa chini,