
Kabla ya kuendelea labda tuweke sawa kwanza hapa, tunaposema ''calculator'' zaidi ya moja ni kwa maana hautakuwa na haja ya kununua ''calculator'' zaidi ya moja kwa ajili ya kazi tofauti tofauti mfano Basic Scientific calculators, Graphing calculators, Financial calculators na aina nyingine za calculator
Kuna aina tofauti tofauti za ''calculator'' ipo aina moja ya kwanza ambayo wengi ndiyo tunaitumia inafahamika kama ''Basic calculator'' ambayo hufanya kazi ndogondogo kama vile hesabu za kujimlisha, kutoa, kugawanya na hesabu nyingine za kawaida
Aina nyinginezo za calculators zimegawanyika kutokana na somo au unaweza kusema kazi husika ni kama vile ''Scientific calculators, Graphing calculators, Financial calculators na aina nyinginezo.
Msingi wa yote hayo ni kukufahamisha kuhusiana na hii wavuti ambayo imesheheni zaidi ya calculator ''3517'' ndani yake na ni bure kuitumia, hii inaitwa ''omnicalculator.com'' itakurahisishia sana kwenye kukokotoa kazi mbali mbali.
Picha: GeeksforGeeks