Monday , 9th Oct , 2023

Ubalozi wa Tanzania nchini Israel umesema kuwa hauna mawasiliano na raia wawili wa nchi hiyo wanaokaa eneo la kusini ambalo limeshuhudia mapambano baina ya wanamgambo wa Hamas na jeshi la Israel.

Balozi wa Tanzania nchini Israel, Alex Kallua

Balozi wa Tanzania nchini Israel, Alex Kallua, amesema mpaka asubuhi ya leo Oktoba 9, 2023, ubalozi huo umekuwa na mawasiliano na Watanzania takribani 350 waliopo nchini humo kasoro wanafunzi hao wawili.

"Tunaendelea kuwafuatilia Watanzania wawili ambao ni wanafunzi waliokuwa wanafanya mafunzo kwa vitendo kusini mwa nchi hiyo, tunafanya jitihada za kuwapata kwanza ili kufahamu walipo na hali zao," amesema Balozi Alex