Thursday , 26th Feb , 2015

Askari watano wamejeruhiwa kufuatia vurugu zilizotokea jana baina ya jeshi la polisi pamoja na wananchi katika mji wa Ilula kijiji cha dinginayo wilaya ya kilolo mkoani Iringa pamoja na raia wawili kujeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi Pudensiana Protas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tayari jeshi la polisi linawashikilia watuhumiwa kumi na nane kwa mahojiano huku upelelezi ukiendelea.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 4 asubuhi na limesababisha kifo cha mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwanne Mtandi na katika vurugu hizo kumesababisha uharibifu wa mali za jeshi la polisi ambayo ni gari, pikipiki pamoja na gari moja ambayo ilikuwa ni kielelezo katika kituo pamoja na kuharibu jingo la polis kwa kuvunja vioo.

Aidha kamanda amesema kuwa fujo hizo zilisababishwa na operesheni kuhusu uuzaji wa pombe za kienyeji na makosa mbalimbali kwa wananchi huku akiwataka wananchi kutokujichukulia sheria mkononi ili kuepusha majanga kama hayo.