Sunday , 24th Sep , 2023

Mkutano wa siku tatu wa Kimataifa kuhusu zao la kahawa duniani, ambao uliandaliwa na asasi ya kimataifa ya Fair Trade, inayosimamia biashara ya haki uliofanyika mjini Bonn nchini ujerumani umemalizika .

Kahawa

Ressy Mashulano, ambae pamoja na kuwa mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Kahawa cha Kagera, (KCU) lakini pia mwakilishi wa Afrika katika mkutano huo katika mahojiano yake na DW amesema kuwa si kila mzalishaji wa kahawa nchini tanzania ni mwanachama wa biashara ya haki(fair trade).

Kwa miaka kadhaa sasa asasi hiyo imekuwa mkombozi wa wakulima wa kahawa kwani inapotokea bei ya kahawa kwenye soko la dunia ikawa imeshuka inaongeza ili kumlinda mkulima, licha ya hayo yote asasi hii imekuwa ikitoa elimu kwa wakulima wa zao hilo pia mikopo nafuu kwani imeamzisha  SACCOS zinazo muwezesha mkulima kupunguza ukali wa maisha pale ambapo kahawa yake haujaingia sokoni.

Kuhusiana na mwenendo wa soko kiujumla kwa bara la Africa amesema bado matumizi ya kahawa ndani ya Africa yapo chini akitolea mfano Tanzania ambapo asilimia 95 ya kahawa lnayo zalishwa inauzwa nje ya nchi huku akisema soko la ulaya lipo vizuri na bado uhitaji wake ni mkubwa.

Kuhusiana na malengo ya wazalishaji wa zao hilo nchini Tanzania amesema malengo yaliyopo kufikia mwaka 2025 ni kuweza kuzalisha tani laki tatu na ili kuyafikia malengo hayo serikali inagawa miche bure kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji zaidi.

''msimu uliopita serikali  kushirikiana na vyama bodi ya kahawa, kushirikiana an TACRI pamoja na mashirika ya nje bila kusahau vyama vya ushirika kama sisi KCU imegawa takribani miche milioni 20 na huu utakuwa muendelezo na mwaka huu tutagawa tena miche milioni 20 kwasababu miche tayari imezalishwa bodi imeshatoa pesa serikali nayo imetoa pesa'' Amesema Ressy Mashulano.

Hata hivyo kahawa inatarajiwa kuongeza pato la Tanzania zaidi kwani ni moja ya mazao ya kimkakati na kibiashara yanayozalishwa Tanzania na yenye kuingiza fedha za kigeni mazao mengine ni pamoja na chai,korosho kokoa na Mkonge.