Monday , 18th Sep , 2023

Klabu ya Simba na Yanga zinataraji kuweka wazi mipango yao kuelekea michezo ya marudiano ya mkondo wa pili hatua ya mwisho ya mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi michuano ya klabu bingwa Afrika msimu huu wa mwaka 2023-24.

Yanga imepata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Al-Merrikh ya Sudan ugenini ilhali Simba SC wao wametoka sare ya 2-2 dhidi ya Power Dynamos ugenini nchini Zambia. Yanga SC tayari imesharejea nchini ilhali Simba SC inataraji kurejea Jumatatu ya leo Septemba 18, 2023 kuanzia saa 8 mchana.

Wawili hao wamesema wataweka wazi harakati zao za maandalizi ya michezo yao ya marudiano huku kili timu ikionekana kujiamini kutokana na matokeo waliyoyapata kwenye mchezo wao wa kwanza.