Monday , 7th Aug , 2023

Kufuatia ajali ya lori la mafuta kuungua moto siku ya jana eneo la Ubungo Kibo Dar es Salaam, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kinondoni limesema kuwa zaidi ya lita elfu 20 za mafuta ziliokolewa kati ya lita elfu 39,500 zilizokuwa ndani ya lori hilo.

Lori liliwka moto Ubungo

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kinondoni Mrakibu Mwandamizi Elisa Mugisha, amesema pia takribani vibanda 19 vya wafanyabiashara vilivyokuwa vimeshika moto viliokolewa huku pikipiki mbili zikiteketea.

"Moto wa mafuta una taratibu zake kwenye uzimaji, kazi kubwa tuliyoifanya ni kupoza tanki ili kuepusha lisilipuke na tulifanikiwa kazi hiyo,"amesema Kamanda Kamugusha.

Aidha Kamanda ameongeza kuwa "Ajali haina kinga, ajali haimtaarifu mtu ukiona kuna shida ni vyema kupiga simu kwa watu wa uokoaji ili wafike kutoa msaada kuliko kuishia kurekodi video na kusambaza sio utamaduni,".