Wednesday , 26th Jul , 2023

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Mtwara imemhukumu miaka 13 jela Shaibu Ally Mtepa mkazi wa Tandahimba kwa kosa la kumkata viganja vya mikono aliyewahi kuwa mke wake Fadina Musa.

Fadina Musa.

Imeelezwa kwamba Desemba 3, 2021, Fadina alifika kwa aliyekuwa mumewe huyo kwa ajili ya kupata mgao wa mali baada ya wanandoa hao kuachana na mahakama kuamua kwamba wagawane mali walizochuma pamoja, ambapo mume alitoka na panga na kumkata viganja mwenzake.

Akizungumza kwa uchungu mara baada ya kusikia hukumu hio Bi Fadina Musa ameona bado hukumu hio ya miaka 13 jela haitoshi kwa jinsi ambavyo anateseka kwa shambulizi alilofanyiwa.

Wakili aliekuwa akimtetea Shaibu Ally Mtepa, Alex Mselenge, ameeleza mteja wake amekiri kosa na kujutia kwa yale ameyafanya na hakuleta usumbufu wowote kwa mahakama na ataongea nae na kushauriana kuona nini wanaweza kufanya.