
Akizungumza na EATV saa moja Kocha Mkuu wa timu hiyo Bakari Shime amesema mechi ilikua nzuri licha ya kwamba wachezaji wake wamecheza chini ya kiwango jambo ambalo amelifanyia kazi na katika mchezo wao kesho julai 27 ,2023 dhidi Ethiopia watakwenda kufanya maajabu.
“Leo tumefanya mazoezi ya kutafuta utimamu wa mwili kwa wachezaji kuwaelekeza makosa mbalimbali ambayo wamefanya jana na kuwataka wapambane katika kuhakikisha wanafanya vyema katika hatua hii ya makundi”amesema Bakari Shime .
Vile Vile Kocha Shime ametoa maoni ya juu ya timu za Afrika kuanza vibaya michuano ya kombe ya dunia ambayo yanafanyika katika nchini New Zealand na Australia.
“Ni ndoto ya kila mwalimu siku moja kucheza kombe la dunia hivyo nina mtihani mkubwa wa kuhakikisha siku moja na sisi tunakwenda kushiriki “amesema Bakari Shime .
Mashindano hayo yanajumuisha nchi tano kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambazo ni Uganda, Ethiopia, Burundi, Zanzibar na Tanzania ambaye ni mwenyeji wa mashindano hayo kwa mwaka huu